MAONI

Nadharia ya Kiswahili

Jancan Limo, Education Consultant & Gilbert Kosgey, Guest Kiswahili Teacher

17 November 2017

Kiswahili ni mojawapo ya lugha ambazo huzungumzwa nchini Kenya. Kiswahili kwa wengi, ni lugha ya pili, ila kwa jamii  kadhaa ni lugha ya kwanza. Kiswahili hutumika kama lugha rasmi na lugha ya taifa nchini Kenya na ni kati ya masomo lazima katika shule ya msingi na upili. Katika nadharia hii, tunajaribu kuorodhesha malengo makuu ya kufundisha lugha ya Kiswahili. Maoni yenu yakaribishwa.

Kiswahili kama lugha rasmi ya Kenya, hufanikisha mawasiliano miongoni mwa kabila tofauti tofauti nchini Kenya, hivyo basi kukuza na kuboresha ushirikiano na umoja miongoni mwa jamii mbalimbali kupitia nyanja mbalimbali kama vile; kidini, biashara, uchukuzi, michezo na hata kupatanisha jamii yenye migogoro.

Kiswahili kama lugha ya taifa hutumika katika kuboresha utendakazi na kuhakikisha kwamba kila mwananchi nchini Kenya amepata huduma bora na kujumuishwa katika ujenzi wa taifa haswa katika shughuli za rasmi bungeni, mahakamani, shuleni na ofisini kuboresha kwa manufaa ya kila mwananchi.

Jancan Limo na Gilbert Kosgey wakiwa Walimu katika shule ya upili mjini Marsabit.

Picha kutoka Mchuma Riziki, Facebook

Hali kadhalika, Kiswahili huwezesha wanajamii kuwa wabunifu,kutafakari na kujieleza kwa wazi na kimantiki bila woga kwani ni lugha nyepesi na rahisi kueleweka.

Aidha, Kiswahili husaidia msomaji kujifunza na kuelewa desturi na itikadi mbalimbali za kijamii kwa kutumia Kiswahili. Hii hufanikishwa kwa kujifunnza chimbuko ya lugha ya Kiswahili na jinsi ufanisi wake ulichangiwa na jamii mbalimbali nchini haswa jamii za mwambao wa pwani.

Kwingineko, Kiswahili humwezesha mtu kuwa na utambuzi kwa mambo yanayohusu na yanayoathiri jamii kwa mfano: teknolojia, siasa, usawa wa jinsia,uchafuzi wa mazingira, haki za watoto, ukimwi miongoni mwa maswala mengine ibuka katika jamii na haswa jinsi ya kukabiliana na changamoto na madhara hasi yanayoletwa na maswala haya ibuka.

“Kwa hakika, lugha ya Kiswahili ni uti wa mgongo na mnara wa jamii kwani imechangia pakubwa katika kuendeleza na kujenga jamii ya sasa.”

Kiswahili humpa mtu uwezo wa kudumu wa kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika ipasavyo kwa lugha ya Kiswahili; mathalan, kuandika barua, kumbukumbu, ripoti, kusikiliza habari za Kiswahili, kusoma magazeti, majarida na vitabu vya hadithi na hata kutoa hotuba kwa hadhira kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Kiswahili humpa msomaji motisha wa kufurahia kujisomea na kujiendeleza mwenyewe kitaaluma kadiri ya uwezo wake. Hii inatokana na kutathmini, kufurahia na kujivunia Kiswahili kama lugha ya taifa na kimataifa kwa kuiga mfano wa magwiji na wataalamu wenye haiba na ushawishi mkubwa kwenye jamii katiaka vitengo kama vile; uanabari, uandishi wa vitabu, usanii miongoni mwa nyanja mbalimbali katika jamii.

Kwa hakika, lugha ya Kiswahili ni uti wa mgongo na mnara wa jamii kwani imechangia pakubwa katika kuendeleza na kujenga jamii ya sasa yenye misukosuko na changamoto ya maswala ibuka katika jamii.Aidha, ni lugha inayokuwa kwa kasi na kutumika kitaifa na hata kimataifa.

Share your thoughts

 
 

Never want to miss a thing? Join our mailing list.

Contact Form Website

Related Articles

Learn, Forget, Learn

I don’t need to be socratical or a psychologist neither do I need to attend any science class in order to make this crystal observation. Metric tonnes of patience has been consumed and a lot of calories have been burnt already. I don’t know how to express what most employers have been through.

A new approach to teaching language in Kenya

Kenya’s curriculum requires that a student going through the 12 years of basic education learns English and Kiswahili every single school day. How is it then that at these language subjects are usually the worst performed during the national exams?